Kwa nini kuwa kijani?

Kwa nini tunahitaji kuwa na mtindo wa maisha ya kijani? Dunia yetu hii ndo makazi yetu pekee, na itabaki kuwa makazi pekee kwa watoto na wajukuu wa familia zetu na jamii. Tunahitajika kulinda makazi yetu na kuhakikisha ni makazi mazuri kwa ajili yetu sisi kama wanadamu, na viumbe vyote hai vinavyoishi.

Dunia inafanya kazi katika mzunguko na imekuwa na uwiano sawa kwa miaka millioni kadhaa. Gesi ambayo wanyama wamekuwa wakivuta pumzi ndiyo gesi hiyohiyo ambayo mimea imekuwa ikitoa pumzi. Uchafu wa kiumbe hai mmoja ni chakula cha kiumbe hai mwingine vivyohivyo na kinyume chake. Maji yanahama kutoka nchi kavu kwenda angani na kurudi tena nchi kavu. 

Sisi kama binadamu tunaharibu mizunguko hii na kuitoa dunia katika uwiano wake. Tunafikiria tu juu ya wakati uliopo na si wakati ujao. Dunia hii ni mahali petu pekee. Tunasababisha matatizo kwa maisha ya binadamu wa sasa na wa baadae, na tunaharibu bayoanuai, yaani viumbe hai tofauti wa duniani.

Ukurasa unaofuata: Matatizo makubwa

 

Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social