Matatizo makubwa yanayotukabili kipindi hiki katika mazingira ni kama mabadiliko ya tabia ya nchi, takataka, na kutokomea kwa baadhi ya viumbe hai.
Mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na “hewa chafu zinazokamata miale ya jua” (greenhouse gases) zinazoongezeka katika tabaka la hewa, katika viwango ambavyo havikuwepo kwa miaka milioni kadhaa. Gesi hizi zinajumuisha kabondaioksaidi na methani. Gesi hizi zinakamata joto la jua katika tabaka la hewa la dunia. Hii inasababisha zaidi majanga yatokanayo na hali ya hewa mbaya, kama dhoruba, mvua kubwa, na upepo mkali. Inasababisha mafuriko katika baadhi ya sehemu, na ukame uliopitiliza katika baadhi ya maeneo. Inayeyusha barafu na inasababisha kiwango cha maji katika bahari kupanda. Hii inasababisha matatizo makubwa kwetu kama binadamu, haswa kwa watu maskini na watu wanaoishi kwenye mazingira hatarishi. Pia inasababisha kutokomea kwa jamii mbalimbali za viumbe hai.
Sababu kuu za gesi zinazonyonya miali ya jua kuongezeka kwenye tabaka la hewa ni kama zifuatazo:

Kuchoma fueli za mabaki ya viumbe hai wa kale: Fueli za mabaki ya viumbe hai wa kale ni fueli zilizotengenezwa mamilioni ya miaka iliyopita. Ni pamoja na makaa ya mawe, mafuta ya petroli, na gesi ya asili. Watu wanachoma fueli hizi ili kuzalisha umeme, kuzalisha bidhaa za viwanda ikiwa ni pamoja na mbolea ya bandia, kwa usafiri wa bidhaa na wa watu, na kwa kupikia na kuotea moto. Wakati tunapoondoa na kuchoma fueli hizi tunatoa kabondaioksaidi (carbon dioxide) ambayo haijawahi kuwepo katika tabaka la hewa kwa mamilioni ya miaka nyuma, kwa kiasi ambacho mzunguko wa kabondaiokaidi hauwezi kunyonya kwa haraka tena. Kabondaioksaidi inayotolewa na fueli hizi leo, hukusanywa na tabaka la hewa, na itasumbua uwiano wa kabondaioksaidi kwa maelfu ya miaka ijayo.

Ukataji wa miti: Mimea huvuta kabondaioksaidi, na kwa kutumia jua, huibadilisha kuwa kaboni ambayo huhifadhiwa katika mti, ambayo huoza na kuingia kwenye udongo. Miti, zaidi ya mimea mingine, ni yenye ufanisi zaidi katika kuchukua kabondaioksaidi kutoka tabaka la hewa. Wakati ambao ardhi iliyokuwa na miti mingi itakapokuwa haipo tena, kabondaioksaidi ndogo inatolewa kwenye tabaka la hewa, ambayo inavuruga mzunguko wa kaboni, na kusababisha wingi wa kabondaioksaidi kwenye tabaka la hewa kuongezeka.
Uchakataji kemikali: Utengenezaji simenti pia unatengeneza kabondaioksaidi kikemikali kutoka kwenye chokaa, pamoja na kabondaioksaidi kutoka kwa fueli.

Methani: Wanyama wenye matumbo manne (“ruminant”) kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo, hutengeneza kiasi kikubwa cha methani wakati wa kula. Watu wanapofuga idadi kubwa ya ng’ombe, kiasi cha methani kwenye tabaka la hewa huongezeka. Methani pia inatokana na kilimo cha mpunga, lakini kwa kiasi kidogo kuliko ufugaji wa ng’ombe.
Takataka

Baadhi ya takataka ni sehemu ya mizunguko ya kawaida ya asili – hizi huitwa taka zinazooza. Vitu vinavyooza (ni kama mabaki ya chakula, maganda, majani, karatasi, mbao na takamwili za binadamu na wanyama) hubadilika na kuwa udongo na huwa ni nzuri kwa kuboresha udongo. Kuna ambazo huoza haraka kuliko nyingine.
Baadhi ya takataka kama madini huwa hayaozi, ila ni sehemu ya ganda la dunia. Kwa vyovyote vile kurudia kuyatumia, au kurejeleza, ni mambo muhimu katika kuhakikisha elementi za madini zinabaki kwa vizazi, na kupunguza uhitaji wa madini mapya na uchimbaji uliopindukia.
Plastiki si kitu asilia, bali huzalishwa na watu kwa kutumia mafuta, na hizi hubakia kama plastiki au vipande vya plastiki kwa mamia ya miaka, au zikichomwa moto huwa zinatoa hewa hatari inayoingia katika tabaka la hewa. Utumiaji mara moja wa plastiki inamaanisha plastiki iliyotengenezwa inatumika mara moja au mara mbili halafu ikatupwa. Kwa utumiaji huu wa mara moja utakuja kupelekea plastiki kuchafua ardhi, kuchafua tabaka la hewa, na mbaya zaidi, kuchafua bahari, kwa vipande vya plastiki hatarishi na sumu, kwa maelfu ya miaka. Daresalaam ni jiji lililopo pwani, na sisi wakazi tuna wajibu wa kuzuia plastiki zisiingie baharini, ambapo vipande vya plastiki huweza kuliwa na samaki na viumbe wengine wa baharini.

Kutokomea kwa baadhi ya viumbe hai / Kupotea bayoanuwai
Kuna aina milioni kadhaa za mimea, wanyama, na viumbe mbalimbali duniani. Hii inaitwa bayoanuwai. Wanasayansi wanajifunza vitu vipya kila siku kuhusu mifumo mbalimbali ya viumbe, na uelewa wa haya umetusaidia sisi kwa namna nyingi kama kutuwezesha kupata madawa, na kuzalisha chakula. Kwa hiyo binadamu wanaharibu bayoanuwai (viumbe hai) vya dunia kuliko hata tunavyoweza kujifunza. Hata zamani watu na viumbe vingine vilikufa na kupotea (iliitwa kutoweka) na viumbe vingine viliibuka. Hata hivyo binadamu wa sasa tumesababisha viumbe kutoweka haraka zaidi kuliko hata miaka milioni nyingi zilizopita.
Ukurasa unaofuata: Unachoweza kufanya
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
