Kwa Tanzania, umeme huzalishwa mara nyingi kwa maji, na uchomaji wa fueli zitokanazo na mabaki ya viumbe hai wa kale, kama mafuta na gesi. Umeme wa maji hautoi kabondaioksaidi, ila gesi inatoa, na mafuta ndiyo mabaya zaidi kuliko hata gesi. Kwa kupunguza matumizi ya umeme, unakuwa pia umepunguza uchomaji wa fueli zitokanazo na mabaki ya viumbe hai wa kale.
Matumizi makubwa ya nishati ni katika kupashia au kupooza. Kwa Dar inamaanisha mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na mtindo wa majengo, epuka matumizi ya viyoyozi (AC), upikaji kwa ufanisi, upashaji wa maji kwa jua, na kupunguza na kuhakikisha ufanisi wa pasi na mafriji/mafriza.
Ujenzi na kiwanja

Upoozaji jengo – Ukipata nafasi ya kuchagua au kujenga makazi – chagua/jenga nyumba yenye mfumo asili wa kupitisha hewa (mfano nyumba zenye uwa (courtyard) na za mtindo wa kiarabu) na iache miti iliyokomaa nje, bila kuikata, kuongeza kivuli. Majengo mazuri yaliyojengwa Dar kabla ya viyoyozi (AC) havijagunduliwa, yalibuniwa namna hii – tujifunze kupitia majengo haya! Wakazi wengi wa Daresalaam wanaishi na kufanya kazi bila viyoyozi. Feni pia zinatumia umeme, ila kiasi kidogo kuliko viyoyozi. Kama una feni au viyoyozi vizime wakati ambao huvitumii, vitumie muda mchache zaidi, na zima kabisa wakati wa majira yasiyo na joto.
Vifaa vya ujenzi – Punguza matumizi ya simenti ambayo inatoa kiasi kikubwa cha kabonidaioksaidi kikemikali na pia inatumia fueli nyingi zitokanazo na mabaki ya viumbe hai wa kale. Una ulazima wa kutengeneza ukuta wa uwa wako kwa simenti? Fikiria kuhusu uzio wa mianzi au uzio wa waya au kupanda mimea kuzunguka/michongoma badala yake! Chokaa za hapa hapa ni machaguo mengine ambayo yanachangia kwa kiasi kidogo zaidi cha utoaji kabonidaioksaidi.

Bustani na miti! – Kama umenunua eneo kwa ajili ya nyumba yako ya kuishi au biashara, na eneo lina miti mikubwa, usiikate – huwa inachukua miongo kukua! Angalia ukaaji mwingine wa jengo unalojenga ili kupunguza miti utakayoikata! Jitahidi kuacha uoto asilia kadiri uwezavyo. Kama hamna miti, panda! Miti itakupatia kivuli na mazingira mazuri kwa jengo lako, huwa inasaidia kunyonya kabondaioksaidi, na majani yake ni virutubisho vya udongo.
Mapishi
Mapishi yana matokeo hasi katika mazingira – uzalishaji wa mkaa wa kuni kwa Daresalaam unahusisha ukataji misitu; gesi na mafuta ya taa ni fueli za mabaki ya viumbe hai wa kale (mafuta ya taa ni shida kuliko hata gesi); na umeme pia huzalishwa kwa upande fulani na fueli za mabaki ya viumbe hai wa kale.

Mkaa unaotokana na taka za mazao ya kilimo badala ya kuni, au mkaa unaotokana na misitu iliyodhibitiwa vizuri, inaweza kuwa uchaguzi mzuri. Kampuni zinajihusisha na mkaa hiyo ni kama “Mkaa mkombozi”, “Mkaa mbadala” na “Mkaa wa Idris” . Kama unatumia mkaa kupikia, tumia jiko lenye ufanisi kama “Jiko bora”.

Kupika katika jiko lilobuniwa vizuri kiufanisi katika kutumia kuni, na kutumia matawi ya miti (si kukata miti mzima) ni chaguo zuri. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu majiko yenye ufanisi ya kuni na mkaa Tanzania kwenye shirika la TaTEDO.
Unaweza kuongeza kiasi cha vyakula visivyohitaji kupikwa katika mlo wako, kupikia watu wengi kwa wakati mmoja na kutumia majiko yenye ufanisi.

Fikiria kujipatia sufuria la jiko la presha – huwa mazuri kwa vyakula kama viazi, maharagwe, wali na mboga mboga. Unapikia kwa muda mpaka mvuke utapoanza kutoka, halafu utafungulia koki na achia gesi/umeme kwa dakika chache zaidi kabla ya kuzima gesi/umeme, na sufuria lenye jiko la presha litaendelea kupika chakula chako hata baada ya jiko lako kuzima kwa muda! (unaweza hata kusikia mapishi yanavyofanyika).
Pika ukiwa umefunika kutunza joto, na usipike kwa kupoteza muda mwingi pasipo ulazima. Loweka maharagwe usiku ili kupunguza muda kuyapika. Kama huli kwa haraka, weka chakula chako kwenye chombo cha kuhifadhia joto kama hotipoti. Kama unaandaa chai au kahawa, usichemshe maji mengi kuliko uhitaji wako, na kuyaweka kwenye chupa ya chai.
Kupasha maji
Kupasha maji ya bafuni – Watu wengi Daresalaam huogea maji ambayo hayajapashwa na ni jambo linalowezekana kabisa katika hali ya hewa kama ya hapa. Kama unataka kuogea maji ya moto – nunua hita inayotumia nishati ya jua. Hivi ni vifaa vinavyotumia joto la jua tu kupasha maji kwa nyuzijoto za juu, bila hata utoaji wa kabonidaioksaidi kabisa, na vinafanyakazi vizuri kabisa hali ya hewa kama hii yetu ya jua. Pia inakuokolea hata fedha kadiri muda unavyoenda – hakuna haja kutumia gesi au umeme kupashia maji kwa ajili ya bafuni/kuogea!

Umeme

Paneli za sola, si majenereta! Sola paneli za PV za kuzalisha umeme zinazidi kuwa bei rahisi, na hazitoi kabonidaioksaidi katika matumizi. Majenereta ya umeme yanagharimu zaidi, yanapiga kelele na yanachafua hewa kwenye eneo husika, na yanatoa kabondaioksaidi nyingi – epuka kutumia jenereta na tumia sola paneli baadala yake. Fikiria kuhusu uwezo wa kudumu ununuapo betri. Betri za sola zenye ubora ni muhimu. Paneli za sola zinaweza hufanya kazi kwa miongo na miongo bila kuhitaji kurekebishwa au hata kununua nyingine. Mifumo ya sola ina utofauti – kuna ile mikubwa inayoweza kuendesha vyombo kama mafriji na feni, na mifumo ya kati inayoweza kutumika kwa ajili ya mataa mengi na kuchaji laptop na simu, na mifumo midogo kutembea nayo ya taa moja na kuchaji simu. Kama unataka kufunga mfumo wa kati au mkubwa, italeta maana zaidi kama utatumia mataa na vifaa vya DC (mkondo wa moja kwa moja) vinavyotoa nishati moja kwa moja kutoka katika betri yako, badala ya kununua kifaa cha kubadili mkondo (AC) kwani hiyo itafanya kuna nishati ipotee wakati wa kubadili mkondo kutoka mkondo wa moja kwa moja (DC) kwenda mkondo unaobadilika (AC).

Chagua vifaa vya umeme vinavyofanya kazi kwa ufanisi – wakati wa kununua vifaa vya umeme, zingatia ufanisi wa nishati. Hii ni ngumu kwa Tanzania ambapo hakuna mfumo rasmi wa kupangilia ufanisi wa vifaa. “Watts” za bidhaa zinapima uwingi wa umeme unaotumika na kifaa kwa sekunde, wakati kifaa kinatumika. Kwa friji, ni muhimu kulizuia kupoteza ubaridi – tumia vizibio vya mlango. Pia zingatia ukubwa – usitumie umeme kupoozea friji au friza kavu – labda friji dogo itafaa kwako!
Tumia vifaa mara chache, au kwa ufanisi –
- Vizime muda ambao havitumiki
- Punguza kama unaweza
- Usiache milango ya friji au friza wazi
- Usitumie kiyoyozi (AC) wakati milango au madirisha ya vioo yakiwa wazi
- Ziba panapovujisha na tunza maji – nishati ilitumika kuyaleta mpaka hapo kwako, kwa hiyo usiyapoteze hivi hivi
- Tumia ngazi kama unaweza, badala ya lifti, katika makazi au eneo la kazi, na itakusaidia kuleta ukakamavu wakati huo huo!
Ukurasa unaofuata: Ungana nasi!
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
