Punguza matumizi au tumia tena! Jambo zuri kabisa ambalo unaweza kufanya kuhusu takataka, ni kupunguza uzalishaji wa taka kwanza. Hata zile taka zinazooza, mara nyingi hutumia nishati itokanayo na fueli ya mabaki ya viumbe hai wa kale kuzizalisha na kuzisafirisha, kwa hiyo punguza idadi ya vitu vipya, na visivyo na ulazima, na vifungashio ununuavyo. Kuna kundi zuri la facebook ambalo lina vidokezo vingi kuhusu hili linaloitwa Zero Waste Tanzania.
Punguza taka za chakula! Usinunue vyakula vinavyoharibika haraka kuliko uhitaji wako. Maliza chakula chako, kihifadhi ule baadae au tafuta mtu anayeweza kukila hapo nyumbani! Masalia ya chakula ambayo mtu hawezi kuyala huwa yanaweza kulishiwa kuku au wanyama wengine.
Mbolea (mboji)
Kwa taka zisizoweza kuliwa zinazo weza kuoza kama maganda ya chakula, majani ya bustani, au makaratasi, kuyafanya kuwa mbolea ni njia nzuri zaidi.
Kama ukibadilisha vitu hivi kuwa mbolea, unatengeneza udongo wenye virutubisho muhimu. Kwa upande mwingine, kama unatupa mabaki yako ya chakula pamoja na plastiki na vitu vingine, huwa vinaweza kuzalisha kiwango kikubwa cha methani, na ukichoma moto, mchanganyiko huo unatoa kiwango kikubwa cha kabondaioksaidi.
Kutengeneza kuwa mbolea ni rahisi sana! Taasisi ya kilimo kamilifu kwa vitendo ya Afrika Mashariki (Practical Permaculture Institutes of East Africa) huendesha kozi juu ya utengenezaji wa mbolea (mboji), na unaweza hata kujifunza mtandaoni.

Hakikisha una angalau vyombo viwili vya taka jikoni mwako, kimoja kwa taka zinazooza (unaweza kuamua kutenganisha taka za jikoni na karatasi) na kingine kwa zile zisizooza, na wafundishe unaoishi nao kutofautisha. Hakuna haja ya kufunga taka za chakula na mifuko ya plastiki katika chombo cha taka, suuza tu chombo cha taka baada ya kuweka katika lundo la mbolea.

Kama una bustani, tengeneza lundo la mbolea pale, ambapo huwa unaweka maganda ya chakula na mabaki kutoka katika chombo cha taka, majani yanayofagiwa kwenye njia, na aina mbalimbali za karatasi ambazo zinaweza kusagika haraka (zisizofungashwa na plastiki).

Lundo la mboji linarahisisha, ila kama unataka kutengeneza mbolea katika eneo ndogo, unaweza kufikiria kupata chombo cha mboji kutoka kwa shirika la The Recycler.
Kama unaishi katika jengo la kupanga lenye bustani, unaweza kujadiliana na meneja au wafanyakazi wa jengo jinsi ya uandaaji wa mboji kwa jengo zima.

Pia unaweza kuhusu vifaa vya mboji vya kuweka ndani, kama aina ya Bokashi, kwa uvunjaji/uozeshaji wa taka za jikoni, kama huna uwezekano wa kupata nafasi ya utengenezaji mboji bustanini.
Vyombo vya taka vya BioBuu vinaweza kuwa na matumizi katika ngazi ya nyumbani, zinakuwezesha kuzalisha chakula cha kuku kwa kutumia nzi askari weusi (black soldier flies) ambao hula taka za chakula.
Urejelezaji
Urejelezaji ni chaguo zuri, ila kama umeshajaribu kupunguza na kutumia tena, ambayo ni machaguo mazuri zaidi. Urejelezaji unaweza kuwa wa kutumia nishati, na mara nyingi huwa kuna usambazaji wa vitu vya kurejeleza kuliko uwezo wa kufanya hivyo. The Recycler inajumuisha orodha ya mahali hapa Dar es Salaam pa kupeleka makaratasi meupe, maboksi, chupa za plastiki, makopo, glasi, nailoni za kufunikia, ikiwa ni pamoja na mwongozo wa vitu gani vinakubalika kurejelezwa na ambavyo havitatakiwi.

Utupaji taka sahihi – kupunguza matumizi, kutumia mara nyingi na urejelezaji yote ni bora zaidi kuliko kufukia taka ardhini kwenye dampo au shimo ya taka. Hata hivyo, kufukia taka ardhini ni bora kuliko kuzikutupa hovyo, kuzichoma, au mbaya zaidi kuzitupia baharini. Kuchoma taka huleta kemikali hatari na kabondaioksaidi hewani, huharibu afya zetu na tabia ya nchi. Plastiki baharini hubakia kwa mamia ya miaka, ni pamoja na vipande vidogo ambavyo vinaweza kuwa sumu kwa samaki na ndege, na kuingia katika mzunguko wa chakula (food chain). Plastiki (zikiwemo mirija, ndala/malapa, makasha ya plastiki/maboya, chupa za plastiki, na vifuniko vya chupa za plastiki Rejea: Nipe Fagio) hizi hufukia beach zetu nzuri Daresalaam. Kamwe usitupe plastiki baharini au ufukweni.
Ukurasa unaofuata: Usafiri wako
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
