Punguza matumizi! Nunua kwa uchache! Karibu kila bidhaa ina kiwango fulani cha madhara katika mazingira, kwa hiyo jitahidi kuwa navyo kwa uchache! Haswa jitahidi kununua kwa uchache zile bidhaa ambazo hununuliwa na kutupwa haraka. Wakati unatoa zawadi, badala ya kununa kitu kipya, jitengenezee kutoka katika mazingira asilia, au vitu vya mitumba, au toa muda wako kusikiliza, kuzungumza na kucheza na wengine. Wakati unatumia pesa zingatia kulipia elimu, na huduma za kujiendeleza na matukio yenye madhara kidogo katika mazingira, badala kununua vitu vinavyoonekana.
Nunua na uza mitumba, na toa bure! Kuna makundi ya facebook ambapo watu huuza na kununua bidhaa za mitumba. Recycle / Freecycle Dar es Salaam facebook group ni kundi ya watu kutoa na kupata vitu vilivyotumika bure. Unaweza pia kununua bidhaa za mitumba sokoni (mfano nguo na baiskeli). Kama huhitaji kitu, jaribu kukiuza au kumpatia mwingine ambaye anaweza kukitumia.

Nunua vya nyumbani! Hii inaweza kufanyika kwa chakula na bidhaa nyinginezo pia. Ni vizuri zaidi unavyopunguza usafirishaji unaotumia nishati zitokanazo na fueli ya mabaki ya viumbe hai wa kale. Na mfumo huu utumike zaidi kwa bidhaa unazonunua mara kwa mara.
Epuka bidhaa za kutumika mara moja!
- Betri zina kemikali zinazo chafua mazingira – tumia zinazodumu-zinazoweza kuchajiwa zenye ubora, na si za kutumia na kutupa au za bei rahisi.

- Wazazi wa watoto wanaweza kutumia nepi za kitambaa za kutumia muda mrefu – hizi hata ukiajiri mtu kuzifua, bado utakuwa umeokoa pesa. Unaweza kuagiza nepi za kitambaa kutoka Jollie Reusable, au zinazotengenezwa na kundi la akina Mama “Thamani -Value not Waste” (0757618419) huko Njombe, pia unaweza kuzinunua huko Kariakoo au duka la “usiende kariakoo” karibu na barabara ya Kawawa.


- Wanawake wanaweza kuzingatia matumizi ya pedi za hedhi za kitambaa, au vikombe vya hedhi, badala ya pedi za kutumia na kutupa. Zinafanya kujisikia vizuri sana na pia zinaokoa hela! Chapa zinazopatikana ni kama Jollie Reusable pads, AFRIpads (Wakala wa Tanzania 0767251111), Hedhi Cup (vinapatikana katika maduka makubwa ya dawa – kwa orodha kamili wasiliana na Anuflo Industries), na Lunette Cup (vinapatikana The Pharmacy, Shoppers Plaza, Masaki).

- Kwa kunyolea unaweza kutafuta vifaa vya nyembe vya madini magumu (metali) kariakoo na kubadili sehemu za makali na si kifaa kizima cha kunyolea, kikianza kuwa butu. Hii inaokoa pesa, na pia itapunguza nyembe zenye plastiki za kutumia mara moja. Mbadala wa nyembe na vifaa vya nyembe salama vinapatikana kwa wingi Dar.
Punguza vifungashio – haswa epuka kufungasha kwa plastiki bidhaa unazonunua mara kwa mara. Unaweza kuacha sabuni za maji/jeli za kuogea, na vyombo vya plastiki vya sabuni za kuoshea vyombo, kwa kutumia sabuni za mche kuoga na kuosha vyombo. Kama unanunua bidhaa kama shampoo katika plastiki, jitahidi kuinunua katika chombo angalau cha lita 5 (kama zinazotumika saluni) halafu unaweza kupunguzia katika vyombo vyako vidogo vidogo pale unapohitaji.
Kimetengenezwa kivipi – Fikiria bidhaa imetengenezwa na nini, na nishati gani iliyotumika kuizalisha? Nunua bidhaa zilizotengezwa na vitu asilia kama inawezekana, badala ya plastiki, haswa kama bidhaa ni ya matumizi ya muda mfupi. Baadhi ya metali (madini), kauri (ceramic) na bidhaa za vioo zinahitaji nishati kubwa sana kuzalisha, kwa hiyo hizi zinatakiwa kuwa bidhaa za kutumika muda mrefu.

- Kwa sponchi za kuogea mwili au kuoshea vyombo, fikiria kutumia sponchi za asili zinazooza, kama loofah (dodoki) ambazo zinapatikana katika mitaa mbalimbali ya Dar, na ni zao la miti.
Uwezo wa kudumu na kurekebishika – Pendelea bidhaa ambazo zinadumu na rahisi kurekebishika zinapoharibika, na zitazokaa kwa muda mrefu. Zinapoharibika zirekebishe. Wapo mafundi wengi Dar wa kila aina, kuanzia wa nguo, wa viatu, wa baiskeli, wa samani (furniture) na wa vifaa vya umeme. Kuna maduka/ofisi za mafundi mazuri katikati ya jiji kama Bombay Walla ambalo hurekebisha vifaa karibu vyote vya jikoni. Bidhaa za metali na mbao zinarekebishika Daresalaam kukiwa na wachomeleaji na mafundi seremala wengi.

Matumizi ya nishati – kuna kipengele maalum katika mwongozo huu kuhusiana na matumizi ya nishati; fikiria hili wakati wa kununua vifaa vya umeme.
Ukurasa unaofuata: Takataka zako
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
