Tuna bahati sana kwa Daresalaam kuwa na aina nyingi ya vyakula freshi, vya kikwetu, na vyenye kupatikana kwa karibu mwaka mzima. Tuvitumie vizuri!

Zalisha chakula chako mwenyewe! Kama una nafasi ya bustani, jaribu kujizalishia chakula chako mwenyewe, kwa kutumia kilimo kamilifu (Permaculture). Unaweza kujifunza zaidi kuhusu kilimo kamilfu kwa kupitia mafunzo ya kilimo hicho ukiwa Daresalaam na Zanzibar kutoka katika taasisi za kilimo kamilifu kwa vitendo Afrika mashariki Practical Permaculture Institutes of East Africa. Usitumie mbolea za viwandani kwani uzalishaji wa mbolea za naitrojeni hutumia kiasi kikubwa sana cha nishati kutoka katika fueli ya mabaki ya viumbe hai wa kale. Usitumie madawa ya viwanda ya kuua wadudu waharibifu, kwani yanachafua mazingira yanayotuzunguka, na yanaua viumbe hai muhimu pamoja na wadudu au wanyama waliokusudiwa. Badala yake, mbinu za kilimo kamilifu hutoa mbinu nzuri zaidi za kuimarisha afya ya udongo na kuwadhibiti wadudu/wanyama waharibifu. Kama una eneo kubwa bustani, vile vile unaweza kufuga kuku – kuku wanaweza kujilisha wenyewe kwa wadudu na mboga kutoka katika bustani yako, na kukupatia mayai yenye virutubisho, na pia kukusaidia kurutubisha udongo wako.

Nunua vya kwetu. Jitahidi kutotumia vitu vilivyoingizwa nchini, haswa vyakula ambavyo vimetoka kilomita nyingi sana kufika Dar. Kadiri umbali unapokuwa mkubwa wa chakula kusafirishwa, vivyo hivyo uwezekano wa kabondaioksaidi nyingi kuzalishwa unakuwa mkubwa zaidi, kutoka katika magari ya usafirshaji. Jumlisha na umuhimu wa kuwasaidia wakulima wa nyumbani kwa kununua vya nyumbani Tanzania. Wakati wa kununua katika masoko yetu waulize wauzaji wapi bidhaa zao zimetoka, na waeleze wazi kuwa unapenda kununua bidhaa za hapahapa nyumbani!

Visivyo pitia michakato mingi kutengenezwa ni bora zaidi. Mchakato wa utengenezaji wa chakula hutumia nishati, na nishati hiyo mara nyingi hutokea katika uchomaji wa fueli ya mabaki ya viumbe hai wa kale. Kwa hiyo, chakula kisichopitia michakato mingi katika utengenezwaji, ndivyo vyakula vyenye afya zaidi!
Vyakula visivyohitaji kupikwa ni bora zaidi. Wote tunakula vyakula vilivyopikwa, ila kama unaweza kuwa na vyakula ghafi vingi katika mlo wako, na ambavyo havijapikwa sana, hiyo itapunguza upikaji, ambao uhusisha uchomaji wa fueli ya mabaki ya viumbe hai wa kale (gesi) au ukataji misitu unaotoa mkaa wa kuni. Angalia hapo chini kujionea baadhi ya vyakula poa/vizuri sana vinavyopatikana Dar!

Punguza vifungashio
Mifuko ya plastiki imepigwa marufuku na serikali, ila maduka yanaendelea kutoa aina nyingine za mifuko ya kutumika mara moja, na mifuko ya karatasi. Ukijibebea mifuko ya kitambaa, na vyombo vigumu au mabox ya chakula, katika mizunguko yako ya kila siku, hapo hakutakuwa na haja ya mifuko ya plastiki madukani na hivyo itatupwa kwa kukosa kazi. Unaweza kutumia zaidi ya mara moja vikapu au mifuko ya vitambaa kwa vitu vikubwa na vikavu, na vyombo vigumu kwa vitu vyenye majimaji na vidogo vidogo (mfano samaki, njegere, sukari, na karanga), kwa miaka na miaka.

Baadhi ya vyakula huja vikiwa vimefungashwa, na vingine havina vifungashio. Jaribu kutafuta vyakula visivyo na vifungashio, kama vyakula ambavyo vinapatikana katika masoko yetu ya wazi hapa Daresaalam. Supamaketi, na wauzaji wa vyakula vya kubeba kulia nyumbani, mara nyingi wanafanya ufungashaji usio lazima. Epuka haswa maboya/plastiki nyeupe ambazo huwa na uwezekano mkubwa sana wa kuingia katika fukwe zetu na baharini. Kama utahitaji sana kufungasha chakula chako, basi chagua chakula kilichofungashiwa katika karatasi na siyo katika plastiki.
Vyakula vya kilimo hai
“Kilimo hai” ni kulima kiasili bila kemikali za viwandani. Vyakula vinaweza kuthibitishwa na mamlaka husika kwamba kweli ni vya Kilimo Hai. Tovuti ya Tanzania Organic Agriculture Movement ina taarifa zaidi kuhusu Kilimo Hai.
Wild Flour Café iliyopo Masaki inauza chakula cha kinyumbani ambacho kimetunukiwa cheti cha kilimo hai. Pia hutoa huduma ya kuwafungashia na kusambaza mpaka manyumbani chakula cha kilimo hai – unaweza kuweka oda yako kupitia App ya Wild flour kwenye Android/IOS, au wasiliana nao kupitia , karibu@wildflour.co.tz/0763492848.
Vyakula vya kustaajabisha!

Madafu yalionunuliwa kutoka kwa muuzaji katika baiskeli. Iwe kama madafu au nazi. Huwa nazi/madafu hutoka maeneo ya karibu na Daresalaam, husafirishwa na baiskeli na huwa na vifungashio asilia kwa asilimia 100%, na haijapitia michatato ya viwandani kwa namna yoyote, na hazihitaji kupikwa. Aisee, ni chakula/kinywaji cha kustaajabisha!

Karanga ghafi – Karanga hulimwa hapahapa, hazihitaji sana kupikwa, na zinakupa protini! Muulize tu muuza karanga zipi ni mbichi na zipi ni za kukaanga/kuchemsha, chagua zisizopikwa kama unaweza, na jijazie mfuko wako wa kitambaa, kikapu au kontena lako!
Asali – unaweza kupata asali ghafi ya Kitanzania, katika chombo chako cha kuwekea unachoweza kukitumia mara kwa mara, kutoka kwa Abdulshakur Ayoob – 0756444350.

Matunda freshi, mbogamboga, majani na viungo – haswa vile vinavyoweza kuliwa bila kupikwa – idadi ni kubwa hapa! Nenda tu katika masoko yetu ya mtaani/magengeni, na masoko ya matunda, na ujaribu kujipatia. Soko lililopo mtaa wa Zanaki katikati ya jiji ni sehemu inayopendekezwa zaidi! Mfano ndizi na parachichi zinakupatia nguvu, nyanya na matunda mbalimbali jamii ya machungwa zinakupatia vitamini nyingi, karoti na njegere ni nzuri kwelikweli, tamu na vina afya. Boresha afya yako, na ladha ya chakula chako, na majani mbalimbali, viungo, tangawizi na moringa. Vyote hivi huzalishwa hapahapa na vinapatikana bila vifungashio. Zungumza na wauzaji, na waulize wapi chakula kinapotokea, na waeleze wazi kuwa unapendelea vyakula vya hapa karibu, na vilivyozalishwa kiasili.
Vyakula vingine vizuri
Vyakula vya kuongeza nguvu

Viazi, ndizi mbivu za kukaanga, mihogo, mahindi ya kiasili ya nyumbani, ugali, na uji wa ulezi ni vyanzo muhimu sana vya nguvu mwilini, kwa mazingira ya hapa. Viazi, ndizi za kukaanga, na mihogo vinaweza kupikwa kwa kutumia majiko ya mgandamizo na kupunguza matumizi ya nishati (jiko la presha).
Mikate mara nyingi huzalishwa kwa unga wa ngano ambao huingizwa nchini, na mara nyingi huingizwa kwa mifuko ya plastiki. Baadhi ya tambi kwa sasa huzalishiwa hapa Tanzania, ingawa nyingine huzalishwa kwa ngano iliyoingizwa nchini, huwezi kuupata bila plastiki na hupitia mchakato ambao hutumia nishati. Mahindi mengi ni ya hapa Tanzania (mahindi ya kuchoma, unga wa mahindi). Mahindi yanayofaa kwa bisi yanatoka Marekani, yanayozalishwa kwa njia za uharibifu, lakini ukiulizauliza sokoni, utaweza kupata mahindi yanayofaa kwa bisi ya hapa Tanzania. Mpunga ni chanzo cha hewa ya methani, kwa hiyo jitahidi kupunguza mchele na kuzidisha viazi, ndizi, mihogo, ugali, mahindi ya nyumbani na ulezi. Na kama utanunua mchele jitahidi upate wa hapahapa nchini Tanzania, mfano mchele wa Morogoro ambao ni karibu na Daresalaam.
Vyakula vya protini
Hivi vimetajwa katika mpangilio unaohitajika na mazingira – jitahidi kula vilivyo juu kuliko vilivyo chini!
Njegere na maharagwe ni vyanzo vizuri vya protini, na hupatikana hapa hapa nyumbani, na mara nyingi hupatikana masokoni bila kuwa vimefungwa. Kuna aina mbalimbali za maharagwe ya hapa nyumbani yanayopatikana – yajaribu kuyaonja. Baadhi ya aina za maharagwe hutumia nishati kubwa kupikwa – jaribu kupunguza matumizi haya kwa kuyaloweka usiku kabla hujapika, na angalia kipengele cha mapishi katika mwongozo huu kuhusu jinsi ya kupunguza namna mapishi yanavyoweza kuathiri mazingira.

Korosho faida yake ni kuwa zinatokea hapa hapa kutoka mikoa ya Lindi and Mtwara, hasara inaweza kusababishwa ni kuwa hizi huhitaji joto na nishati wakati wa kubangua, kabla ya kuziuza.

Mayai ni chanzo kizuri cha protini, na yanapatikana katika maeneo yetu, na bila kufungashwa. Mayai ya kuku wa kineyeji yatokanayo na ufugaji huria wa kuku, ambao sana sana hula wadudu ardhini na mabaki ya chakula, ni mazuri sana kwa afya yako na kwa mazingira, na yanapatikana sana Dar! Tumia trei za mayai zile zile, usichukui mpya!
Samaki, kama wamevuliwa bila kutumia baruti, na wavuvi wazawa katika idadi ambayo ni endelevu, ni chanzo kizuri cha protini. Madhara makubwa ya uvuvi kwa mazingira ni nishati ya fueli inayotumika na boti za uvuvi. Uvuvi unaotumia baruti umekatazwa na sheria za Tanzania, ila unafanyika bado. Uvuvi huu unaharibu makazi ya samaki katika matumbawe na unaua samaki wengi zaidi kuliko hata wanaovunwa.
Nyama si rafiki sana kimazingira kuliko vyakula vingine, sababu rasilimali hizi hizi (ardhi, nishati na rasilimali nyingine) huzalisha protini kidogo kwa ajili ya watu kama zinazalisha vyakula vya wanyama ambao watu huwala nyama, rasilimali hizo zingeweza kutumika kuzalisha mimea ambayo ingewapa watu chakula moja kwa moja.
Nyama ya kuku si mbaya sana kwa mazingira kama nyama nyingine, ingawa pia inategemea na kuku hao pia wamelishwa nini. Angalia Biobuu kwa njia mpya rafiki kwa mazingira kuwalisha kuku wako. Ingawa ni vigumu kujua kuku wako amekuwa akilishwa nini.

Mafuta ya kupikia -Nunua mafuta ya alizeti si mafuta ya mawese! Mafuta ya alizeti huzalishwa Tanzania, na yanaweza kununuliwa katika ndoo kubwa, na unaweza kuitumia ndoo kwa matumizi mengine baada ya mafuta kuisha. Kamwe usinunue ndoo tupu – nunua ndoo yenye mafuta ya alizeti badala yake.
Vyakula visivyo vizuri sana
Mafuta ya mawese (ambayo kwa bahati mbaya ndiyo mafuta ya bei rahisi sana hapa Dar) huleta madhara makubwa sana kimazingira, kwa sababu mbalimbali. Mafuta haya huletwa kutoka mbali (kuyasafisha tu ndo hufanyikia Tanzania). Mafuta ya mawese hutokea huko katika mashamba makubwa ya miwese katika maeneo ya Malaysia na Indonesia ambapo misitu mikubwa ya kitropiki inayoleta mvua hukatwa kila siku ili kuzalisha mafuta ya mawese.
Bidhaa za maziwa ya ng’ombe kama maziwa yenyewe, mgando, jibini (cheese) na aisikirimu vyote huleta matokeo hasi ya kuongeza uzalishaji wa methani kutoka kwa ng’ombe na mbuzi. Baadhi ya watu wameamua kuacha moja kwa moja – unaweza kufanya hivyo pia kama unaweza. Hata hivyo kama unakula bidhaa za maziwa, ni jambo linalowezekana kabisa kwenye baadhi ya maeneo ya Dar kupata maziwa kutoka kwa ng’ombe wa hapa Dar es Salaam katika vyombo unavyoweza kuwekea mara kwa mara. Unaweza pia kujaribu kutengeneza mgando wako mwenyewe badala ya kununua katika chupa ndogo ngumu za plastiki za matumizi mara moja inazokuja nazo. Kumbuka jibini huleta kasoro kubwa kimazingira – huletwa kutoka mbali sehemu kama Ireland na New Zealand, inatumia maziwa mengi sana, hivyo hutoaji wa hewa ya methani ni mkubwa katika utengenezaji wa kiasi kidogo tu cha jibini, na ni chakula kilichochakatwa.
Nyama kutoka kwa wanyama wa matumbo manne, kama ng’ombe na mbuzi, hutoa methani nyingi kutokana na mchakato wa mmeng’enyo wa hawa wanyama. Uzalishaji wa nyama pia unaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa misitu, ikiwa ng’ombe watalishwa katika ardhi ambayo miti imekatwa ili wapate malisho, na ng’ombe wanatoa methani kuliko mbuzi. Epuka nyama ya ng’ombe na mbuzi, haswa ya ng’ombe, au punguza kiasi au kurudia rudia kula!
Vinywaji vyako

Maji ya madafu ni kinywaji kizuri sana na cha kustaajabisha! Kina afya, ni cha kinyumbani na kimesafirishwa na baiskeli. Vifungashio vyake ni vya asili, na kwa ujumla ni rafiki kwa mazingira.

Watu wengi hawatakunywa maji ya bomba yasiyo chujwa kwa sababu mbalimbali za usalama. Njia rafiki zaidi kimazingira ni kuyachuja maji yako ya bomba na kuyanywa.
Njia ya pili mbadala ni kununua chupa zenye dispensa ya maji (chupa maalumu za kutawanyia maji) na kuzirudisha. Pia unaweza kujijengea dispensa yako ya maji nyumbani, kwa kutumia ndoo na kuiwekea koki kwa chini -fundi anaweza kukutengenezea. Jaribu kuepuka chupa za maji za kutumia na kutupa.
Juisi freshi zinapatikana kwa wauzaji wa mtaani, zinozotolewa kwa glasi zinazosafishika, au unaweza kuchukua na chupa yako inayoweza kutumika mara kwa mara, hizi zinapendelewa kuliko za viwandani zilizo katika katoni nyingi za plastiki. Kumbuka kuwaambia wasikuwekee mrija wa kutumia na kutupa mara moja ukiwa baa au mgahawani (waelewesha ikiwa hawajakuelewa au hata wakikushangaa)!
Kama unakunywa soda au kilevi, nunua katika glasi za kutumika mara kwa mara. Chupa za plastiki hutumika mara moja, na mbaya zaidi ni chupa za bluu, nyeusi au kahawia, ambazo haziwezi hata kurejelezwa. Makopo ya aluminiamu yanahitaji kiasi kikubwa cha nishati, na haziwezi kutumika tena. Unaweza kuwekeza kwenye chupa za soda au bia na kuzihifadhi nyumbani na kuzipeleka baa kujazwa tena. Kumbuka glasi zinazotumika mara moja (mfano chupa za mvinyo) ni mbaya kwa mazingira kutokana na kiwango kikubwa cha nishati kinachotumika (mara nyingi katika fueli za mabaki ya viumbe hai wa kale) – kiasi hicho kinahitajika kuzalisha glasi kwa matumizi ya mara moja. Katoni za mvinyo zinapendelewa kutumika katika glasi za kutumia na kutupa mara moja.
Ukurasa unaofuata: Unachokinunua
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
