Suluhisho linahusisha kubadlisha mifumo mikubwa, ambayo inayoonekana hatarishi. Bali, mabadiliko makubwa yanaweza kuanza na mabadiliko ya mtu mmoja mmoja. Kila mmoja wetu ana nafasi kutatua haya matatizo kama mwananchi, kama mwanajamii, kama mfanyakazi na katika maisha ya kila siku.

Ukiwa kama raia: Pengine jambo muhimu zaidi unaweza kufanya ni kutumia nguvu yako kama raia. Ongea na wawakilishi wako waliochaguliwa kuhusu masuala ya mazingira, na wajulishe masuala ya mazingira ni muhimu kwako. Jiunga na kampeni na mashirika ambayo yanafanya kazi katika masuala ya mazingira, na fikiria mazingira wakati unapiga kura.
Ukiwa kama mwanakikundi: Sisi sote ni wanachama wa vikundi mbalimbali tofauti kama familia, vikundi vya kiimani, marafiki na makundi mengineyo. Watu wengi bado hawaelewi kuhusu maswala ya kimazingira. Unaweza kutumia fursa kuelimisha na kubadilishana mawazo kuhusu maswala ya kimazingira. Pia unaweza kujiunga na makundi ambayo yanayoboresha mazingira, kama kukusanya mabaki ya uchafu pembezoni mwa bahari (Nipe Fagio) au kupanda miti kwenye maeneo ya kijamii.


Kazi na uwekezaji wako: Kitu kingine unachoweza kufanya ni kuboresha mazingira kupitia kazi yako. Kama ukiwa unaweza kuchagua kazi ya kufanya katika maisha, jitahidi kuchagua kazi inayoweza pia kusaidia kutatua matatizo ya kimazingira, au angalau kufanya kazi ambayo haitahatarisha zaidi mazingira. Unaweza kufanya mabadiliko, na hata kuwashawishi wenzio kubadilika, katika maeneo ya kazi. Kama una pesa za kuwekeza, basi wekeza katika miradi inayoweza kusaidia utunzaji mazingira, na si kuyaharibu.

Katika maisha yako ya kila siku: Kitu kingine unachoweza kufanya ni kuishi kwa mfumo ambao ni rafiki kwa mazingira, na ndilo lengo letu la kampeni hii ya mwongozo wa maisha ya kijani. Mabadiliko kwa moja moja yanaweza kuongezeka, na mabadiliko ya mahitaji ya wateja yanaweza kuathiri biashara na usambazaji wa bidhaa. Kwa kuongezea kuishi maisha yako kwa mfumo rafiki kimazingira ni jinsi ya kuwa mfano bora, na kusaidia mambo mengine matatu ya nini unaweza kufanya hapo juu.
Ukurasa unaofuata: Unachokula na kunywa
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
