Mashirika
- ForumCC ni shirika mama la mashirika mengi yanayo shughulika na mabadiliko ya tabia ya nchi. Unaweza pia kuangalia washirika wake.
- TaTEDO linashughulika na nishati endelevu.
- Nipe Fagio linashughulika na masuala ya takataka, ikiwa ni pamoja na kutetea usafi wa mazingira na kusafisha fukwe.
- Practical Permaculture Institutes of East Africa (taasisi ya kilimo kamilifu ya Afrika mashariki) huwa inawezesha mafunzo ya kilimo kamilifu kwa Zanzibar na hufika mpaka Dar.
- Tanzania Organic Agriculture Movement ina taarifa kuhusu Kilimo Hai
Kurasa na makundi mbalimbali ya Facebook
- Green Dar – ni kundi la facebook la watu waliosoma muongozo huu wa Kijanisha Dar, na wanataka kusaidiana kutekeleza.
- UWABA ni jamii inayojihusisha na uendeshaji wa baiskeli na kuboresha hali na usalama wa waendesha baiskeli.
- Zero Waste Tanzania ni kurasa ya mtandao wa facebook yenye mbinu/vidokezo vya jinsi ya kupunguza takataka.
- Recycle / Freecycle Dar es Salaam facebook group ni kundi la facebook la kutoa na kupokea vitu vya mtumba/vilivyotumika bure.
Bidhaa na huduma
- The Recycler hutoa huduma za urejelezaji na pia huuza vyombo vya kutengenezea mbolea ya mboji.
- Fasta Cycle Messengers hupelekea watu vitu au bidhaa kwa kutumia baiskeli na vyombo visivyo vya moto – 0714132782
- Mkaa Mkombozi – 0769862933
- Ensol na kampuni nyingine nyingi huuza hita za zinazotumia mwanga wa jua kupashia maji na mifumo ya umeme ya jua.
- Abdulshakur Ayoob 0756 444 350 anaweza kukuuzia asali ghafi ya Kitanzania katika chombo chako mwenyewe cha kutumia zaidi ya mara moja.
- Wild Flour Café iliyopo Masaki inauza chakula cha kinyumbani ambacho kimetunukiwa cheti cha kilimo hai. Pia hutoa huduma ya kuwafungashia na kusambaza mpaka manyumbani chakula cha kilimo hai – unaweza kuweka oda yako kupitia App ya Wild flour kwenye Android/IOS, au wasiliana nao kupitia , karibu@wildflour.co.tz/0763492848.
- Jollie Reusable wanatengeneza taulo za hedhi na pia nepi za kitambaa
- “Thamani -Value not Waste” (0757618419) kundi la akina Mama huko Njombe wanaotengeneza nepi za vitambaa za watoto. Duka la Usiende Kariakoo karibu na barabara ya Kawawa pia huuza nepi za vitambaa.
- AFRIpads – taulo za hedhi zinapatikana Tanzania kwa wakala 0767251111
- Anuflo Industries husambaza Hedhi Menstrual Cup (vikombe vya hedhi) katika maduka makubwa ya madawa, na Lunette Cup vinapatikana The Pharmacy, Shoppers Plaza, Masaki.
- Bombay Walla hufanyia marekebisho vifaa vingi vya jikoni.
- BioBuu hutoa vyakula endelevu vya kuku vilivyotengenezwa na takataka za chakula.
Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social
